Thursday, October 18, 2012

REBELO APUUZA SHUTUMA JUU YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL.

Aldo Rebelo.
WAZIRI wa Michezo wa Brazil, Aldo Rebelo amepuuza shutuma juu ya maandalizi ya ya Kombe la Dunia kwamba matatizo yaliyotokea katika michuano ya Olimpiki jijini London yameonyesha kwamba ni vigumu kuandaa tukio kubwa la michezo kama hilo bila kutokea matatizo. Wakati Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lilipotembelea viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia Kusini mwa nchi hiyo , waziri huyo alitoa mifano kadhaa ya jinsi mambo yalivyokwenda isivyotakiwa katika michuano ya London. Rebelo amesema kuwa alilazimika kufuta baadhi ya mahojiano aliyotaka kufanyiwa kutokana na foleni kali iliyokuwepo kipindi huku rais wa mamlaka ya olimpiki jijini Rio de Janeiro naye aliibiwa wakati akiwa jijini humo. Waziri huyo alisema mbali na matatizo hayo lakini pia kulikuwa na tatizo kubwa la mawasiliano pamoja na watu kupoteza mizigo yao lakini hakuna yoyote aliyewashutumu waandaaji au kusema kuwa mashindano hayo hayakufanikiwa kutokana na matukio hayo. Rebelo amekiri kuwa ni kweli ujenzi wa miundo mbinu na viwanja kwa ajili ya Kombe la Dunia unakwenda taratibu lakini aliwahakikishia wakaguzi hao kutoka FIFA kuwa kila kitu kitakamilika kwa wakati.


No comments:

Post a Comment