KLABU ya Lazio ya nchini Italia imetozwa faini ya euro 40,000 kwa tabia ya kibaguzi waliyoonyesha mashabiki wake wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya Tottenham mwezi uliopita. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mshambuliaji wa Spurs Jermain Defoe, winga Aaron Lennon na Andros Townsend aliyeingia kipindi cha pili walikuwa wakipigiwa kelele za nyani ingawa hata hivyo meneja wa Spurs Andre Villas-Boas amesema hakusikia chochote. Mchezo huo wa kundi J ulichezwa Septemba 20 katika Uwanja wa White Hart Lane mbele ya rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini na kumalizika kwa sare y bila ya kufungana. Hivi sasa shirikisho hilo linaangalia uwezekano wa kuongeza adhabu isiwe faini pekee kwa timu ambazo mashabiki wake watakutwa na hatia ya mambo ya kibaguzi ili kujaribu kutokomeza kabisa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment