SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema kuwa viwanja vinne vinaweza kutumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa viwanja vingine ili vitimie sita kama ilivyopangwa. Mkurugenzi wa Mawasialiano wa FIFA Walter de Gregorio amesema kuwa watahitaji vinne lakini wanaweza kutumia viwanja vitano au sita kama vitakuwa vimekamilika kwa wakati kabla ya kuanza kwa michuano hiyo mwakani. Idadi kamili ya viwanja ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano hiyo itajulikana Novemba 8 mwaka huu jijini SaoPaulo ambapo pia watatoa maelezo juu ya suala ya uuzwaji wa tiketi ambao utaanza Desemba 3. Michuano ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kuanza kutimua vumbi June 15 mpaka 30 mwakani katika miji minne ambayo tayari imeshapewa kibali cha kuwa wenyeji. Mchezo wa ufunguzi unatayarajiwa kuchezwa katika mji mkuu wan chi hiyo Brasilia huku fainali ikipigwa katika jiji la Rio de Janeiro huku miji ya Belo Horizonte na Fortaleza kukichezwa mechi zingine.
No comments:
Post a Comment