Friday, October 19, 2012

RUNGU LA CAF LAIANGUKIA ES SAHEL.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetoa hukumu yake kufuatia tukio la mchezo baina ya klabu ya ES Sahel na Esperance zote za Tunisia katika hatua ya makundi uliochezwa Agosti mwaka huu. ES Sahel ambao walifungwa mabao 2-0 katika mchezo huo wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kukutwa na hatia ya mashabiki wake kufanya vurugu na sasa watacheza mechi mbili za nyumbani bila ya mashabiki kuwepo. Mbali na adhabu hiyo klabu hiyo pia imetozwa faini ya dola 25,000 hata hivyo wamepewa ruhusa ya kushiriki Kombe la Shirikisho baada ya uongozi kuhofia kuwa wangeweza kuondolewa pia. Mchezo huo uliochezwa Agosti 18 katika Uwanja wa Olympic jijini Sousse ilibidi mwamuzi aumalize katika dakika ya 70 baada ya mashabiki kuanza vurugu kwa kurusha vitu mbalimbali uwanjani.

No comments:

Post a Comment