Tuesday, October 23, 2012

BAADA YA KUVULIWA UBINGWA SASA ARMSTRONG ADAIWA FEDHA ALIZOSHINDA.

NYOTA wa zamani wa mbio baiskeli, Lance Armstrong atalazimika kulipa fedha alizopata kama mshindi wa michuano ya Tour de France baada ya kunyang’anywa mataji yote saba aliyoshinda baada ya kukutwa na hatia ya kutumia madawa ambayo yamekatazwa michezoni. Muungano wa Kimataifa wa Waendesha Baiskeli-UCI ulimvua ubingwa wote aliopata Armstrong kuanzia Agosti mosi mwaka 1998 Jana. Mkurugenzi wa michuano ya Tour de France Christian Prudhomme alikubaliana na uamuzi wa UCI na kuongeza kuwa sheria za muungano huo ziko wazi kwamba mtu yoyote atakayevuliwa ubingwa atalazimika kulipa fedha alizopewa kama mshindi. Inakadiriwa kuwa Armstrong amepata kiasi cha paundi milioni 2.4 kwa kushinda michuano ya Tour de France katika kipindi cha miaka saba mfululizo kuanzia mwaka 1999 mpaka mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment