Tuesday, October 16, 2012

BIN HAMMAM AIKATIA RUFANI FIFA, CAS.

ALIYEWAHI kuwa mgombea wa zamani wa urais na mjumbe wa kamati kuu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Mohamed Bin Hammam amekata rufani katika Mahakama ya Michezo ya Usuluhishi-CAS juu ya kjufungiwa tena na shirikisho hilo ili kupisha uchunguzi mpya. Bin Hammam ambaye alichuana na Sepp Blatter katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA mwaka jana amefungiwa na shirikisho hilo Julai 26 mwaka huu ikiwa ni wiki moja baada ya CAS kutengua adhabu yake ya kufungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya michezo. Wakili wa Bin Hammam, Eugene Gulland katika taarifa yake alithibitisha kuwa mteja wake ambaye pia amewahi kuwa rais wa Shrikisho la Soka barani Asia-AFC ameamua kukata rufani kupinga adhabu hiyo aliyopewa na FIFA. Katika taarifa yake ya kutengua kifungo cha aisha cha Bin Hammam, CAS katika taarifa imesema kuwa FIFA walishindwa kuwasilisha ushahidi uliokamilika juu ya tuhuma kwamba aliwanunua maofisa wa soka wan chi za Carribean katika uchaguzi mwaka uliopita ingawa walimalizia kuwa uamuzi huo haumaanishi kwamba hakutenda kitendo hicho. Bin Hammam alikuwa natuhumiwa kujaribu kuwanunua maofisa wa soka wa nchi za Caribbean ili waweze kumpigia kura kwa kuwapa bahasha zilizokuwa na kiasi cha dola 40,000 kila mmoja katika mkutano na viongozi hao uliofanyika nchini Hispania mwezi mmoja kabla ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment