Tuesday, October 16, 2012

FSF YAMLAUMU DIOUF VURUGU ZA SENEGAL.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Senegal-FSF, Augustin Senghor amesema kuwa tukio lilitokea katika mchezo Jumamosi iliyopita lilikuwa ni hujuma za makusudi zilizopangwa na watu ambao wanataka kusambaratisha soka la nchini humo na kulitia doa shirikisho hilo. Senghor amesema kuwa mtu binafsi alinunua tiketi na kusisambaza kwa mashabiki wakorofi kwa madhumuni ya kuvuruga mchezo kati ya Senegal na Ivory Coast ambao ulikuwa ni mchezo wa pili wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kitendo ambacho kilifanikiwa kwani mchezohuo uliisha katika dakika ya 76 baada ya vurugu kuzuka. Rais huyo aliendelea kusema kuwa wanaamini kuwa tukio hilo ni la hujuma na lilifanywa na mtu au kikundi cha watu ili kufuruga soka nchini humo. Kauli hiyo ya Senghor inakuwa kama inamlenga mshambuliaji nyota wa klabu ya Leeds United, El Hadji Diouf ambaye mapema Jumatatu alikiri kuwa FSF ilizuia tiketi zake 1,000 alizoagiza kwa ajili ya kusambaza kwa mashabiki wake kwa kuogopa nyota huyo anataka kuwapatia tiketi hizo wahuni ili wavuruge mchezo huo. Kwa mujibu wa chanzo kilichikaribu na FSF, Diouf ndiye pekee aliyelipia tiketi nyingi zaidi katika mchezo huo ingawa mwenyewe amekunusha kuhusika katika kuchochea vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment