Sunday, October 7, 2012

COLE KUCHUKULIWA HATUA CHELSEA.

Meneja wa klabu ya Chelsea, ROBERTO DI MATTEO amefafanua kuwa mchezaji ASHLEY COLE anaweza kupewa adhabu na klabu hiyo baada ya kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiiponda Chama cha Soka cha Uingereza-FA. COLE mwenye umri wa miaka 31 alituma ujumbe mara baada ya Baraza Huru la FA kutoa utetezi wake ambao ulimkuta mchezaji mwenzake JOHN TERRY na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi beki wa Queens Park Rangers ANTON FERDINAND. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo DI MATTEO amesema kuwa klabu hiyo ina sera zake kuhusiana na mitandao ya kijamii hivyo ni wazi kutakuwa na hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa kwa COLE na yeye hataweza kuingilia. Beki huyo wa kushoto alituma ujumbe wa kuitukana FA kwa uamuzi waliotoa lakini baadae aliufuta ujumbe huo ingawa hata hivyo Chelsea imepanga kumchukulia hatua na pia anaweza kupambana na adhabu nyingine kutoka FA. DI MATTEO hajawazuia wachezaji wake kutumia mitandao ya kijamii lakini amewaonya kuwa inaweza kuwaletea matatizo kama wasipotumia uhuru huo vizuri.

No comments:

Post a Comment