Kiungo nyota wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Chelsea, FRANK LAMPARD kuna hatihati ya kutocheza mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya San Morino Ijumaa ijayo baada ya kuumia katika mchezo ambao timu yake iliibuka kidedea kwa kuifunga mabao 4-1 Norwich.
Beki wa klabu ya Arsenal, KIERAN GIBBS naye pia anaweza kuwa nje ya uwanja katika mchezo huo baada ya kutolea nje mapema katika kipindi cha pili wakati timu yake ilipoibika na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United Jumamosi. Katika mchezo wa Chelsea ambao ulipigwa katika Uwanja wa Stamford Bridge, LAMPARD alifunga bao la pili na kufikia rekodi ya BOBBY TAMBLING aliyewahi kufunga mabao 129 lakini alionekana wazi kusumbuliwa na maumivu wakati alipotolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Ramires katika dakika ya 23 ya mchezo huo. Akihojiwa kuhusiana na hali ya mchezaji huyo meneja wa klabu hiyo ROBERTO DI MATTEO kwa muda huo asingeweza kufahamu lakini baada ya madaktari wa timu hiyo kumfanyia uchunguzi ndio watatoa majibu ya nini kinamsumbua kiungo huyo. Kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo ROY HODGSON ambaye alikuwepo uwanjani hapo kuwafuatilia LAMPARD na ASHLEY COLE atakuwa na amepatwa na mfadhaiko baada ya kumuona nahodha wake huyo ambaye amechukua nafasi ya STEVEN GERARD anayetumikia adhabu kuukosa mchezo dhidi ya San marino.
No comments:
Post a Comment