Monday, October 15, 2012

ETO'O ALAUMU MAANDALIZI MABOVU YAMECHANGIA CAMEROON KUTOLEWA AFCON.

MSHAMBULIAJI nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o amelaumu maandalizi mabovu ndio yaliyochangia timu yao kushindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini 2013. Pamoja na ushindi waliopata wa mabao 2-1 dhidi ya Cape Verde mchezo ambao uliochezwa jijini Younde kikosi hicho kilishindwa kufuzu baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa ugenini dhidi ya timu hiyo iliochezwa jijini Praia. Eto’o ambaye ndio amerejea katika kikosi hicho baada ya msuguano na maofisa wa soka nchi hiyo kumalizika alishindwa kukisaidia kikosi chake kufuzu michuano hiyo. Akihojiwa mara baada ya ya mchezo huo Eto’o amesema kuwa kiakili walikuwa na wiki ngumu kabla ya mchezo huo kwakuwa walikuwa wanajua ni lazima wafunge mabao mawili bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa ili waweze kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati lakini walishindwa na kuruhusu wavu wao kutikiswa. Eto’o aliendelea kusema kuwa sasa inabidi wasahau hayo na kuhamishia nguvu zao kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment