Monday, October 15, 2012

DJOKOVIC ALIPA KISASI KWA MURRAY.

MCHEZA nyota kutoka uingereza Andy Murray ameshindwa kunyakuwa taji la tatu mfululizo la Shanghai Masters baada ya kukubali kipigo kutoka Novak Djokovic wa Serbia. Nyota hao ambao wamekutana kwa mara ya kwanza toka Murray anyakue taji la michuano ya wazi ya Marekani, Djokovic alifanikiwa kuibuka mshindi kwa 5-7 7-6 6-3. Katika mchezo huo Murray ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani alionyesha mchezo ambao aliutumia kumuondosha Roger Federer katika hatua ya nusu fainali lakini Djokovic alionyesha kujipanga vyema kulipa kisasi baada ya Murray kumfunga katika michezo miwili iliyopita. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Djokovic amesema kuwa mara nyingi anapokutana na Murray huwa anategemea mchezo mgumu na mrefu lakini anashukuru kwamba safari hii yeye ndio aliyeibuka mshindi.

No comments:

Post a Comment