Monday, October 15, 2012

VETTEL KUITOSA RED BULL NA KUHAMIA FERRARI.

BINGWA mara mbili wa dunia wa michuano ya langalanga, Sebastian Vettel anajipanga kujiunga na timu ya Ferrari mwaka 2014 huku Filipe Massa akibakia katika timu hiyo ya Italia kwa mwaka ujao. Chanzo kutoka ndani ya Ferrari kilihabalisha kuwa Vettel mwenye umri wa miaka 25 tayari amesaini mkataba na timu hiyo kwa ajili ya kijiunga mwaka 2014 lakini itategemea na matokeo ya timu hiyo. Vettel ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Fernando Alonso mwenye umri wa miaka 31 ambaye toka ajiunge na timu hiyo baada ya kunyakuwa taji la dunia akiwa na timu ya Renault mwaka 2005 na 2006 ameshindwa kutamba akiwa na Ferrari. Vettel ambaye kwasasa yuko timu ya Red Bull ndio anaongoza akiwa na alama sita zaidi ya Alonso katika kinyang’anyiro cha kufukuzia taji la dunia msimu huu.

No comments:

Post a Comment