Thursday, October 25, 2012

ETO'O AMPONDA SONG.

MSHAMBULIAJI nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o amemkosoa mchezaji mwenzake Alex Song kwa kudai kuwa hajafikia kiwango cha mchezaji nyota wa dunia. Eto’o mwenye umri wa miaka 31 ambaye anakipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini Urusi amekuwa na uhusiano usio wa kuridhisha na kiungo huyo wa Barcelona toka Song alipokataa kushikana mikono naye katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal mwaka uliopita. Akihojiwa na luninga moja nchini Ufaransa kama nyota hao wana mgogoro unaoendelea, Eto’o amesema kuwa hakuna mgogoro unaondelea kati ya nyota wawili kwani yeye ni mmoja wa wachezaji bora duniani na Song hata Cameroon sio mmoja wa wachezaji bora. Wachezaji hao walionekana kama wamshamaliza matatizo yao katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde lakini Eto’o ana wasiwasi kwamba hakutaweza kuwa na maridhiano baina yake na Song. Tetesi zinasema kuwa uhasama wa wachezaji umeongezeka kutokana na Song kutaka kumnyang’anya kitambaa cha unahodha Eto’o ambaye alifungiwa kwa miezi nane baada ya kushawishi wachezaji wenzake kugoma wakidai posho zao. Eto,o amenyakuwa tuzo ya mchezaji bora duniani mana nne huku akiwa ndiye mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika katika kipindi chote baada ya kufunga mabao 18. 

No comments:

Post a Comment