Wednesday, October 17, 2012

FA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUWAREJESHEA MASHABIKI WAKE GHARAMA ZAO BAADA YA MCHEZO KUSOGEZWA MBELE.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA huenda kikaangalia uwezekano wa kuwarudishia gharama mashabiki wa soka wa nchi hiyo ambao wameshindwa kubakia nchini Poland kwa ajili ya kutazama mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 baina ya nchi hizo ambao ulisogezwa mbele. Mashabiki wa Uingereza wapatao 2,500 walisafiri kwenda jijini Warsaw kwa ajili ya mchezo wa Jumanne lakini ulihahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji huku mashabiki wengi kati ya hao walikuwa wamekata tiketi za kurejea Uingereza jioni mara baada ya mchezo huo. Msemaji wa FA Adrian Bevington athibitisha kuwa wanaangalia uwezekano wa kurejesha gharama za mashabiki hao lakini asingeweza kutoa uamuzi wa mwisho kwa muda huo. Mpaka sasa haijajulikana ni mashabiki wangapi ambao wataweza kuhudhuria mchezo huo ambao utachezwa baadae leo ikiwa ni muda wa saa 24 toka usogezwe mbele kutoka na uwanja huo kujaa maji.

No comments:

Post a Comment