Wednesday, October 17, 2012

CAF YABADILISHA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MCHEZO WA ESPERANCE NA TP MAZEMBE JIJINI TUNIS.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetaja majina mapya ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Esperance ya Tunisia na TP Mazembe ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC. Hatua hiyo ya CAF imekuja kufuatia TP Mazembe kutuma barua ya malalamiko juu ya mwamuzi aliyetakiwa kuchezesha mchezo huo Bakary Gassama kutoka Gambia. Shirikisho hilo sasa limeamua kumbadilisha mwamuzi huyo na kumpa Badara Diatta kutoka Senegal kuchezesha mpambano huo ambao utapigwa Jumamosi Octoba 20 jijini Tunis. Hata hivyo waandishi wa habari nchini Tunisia wamekuwa wakiponda uamuzi huo wa CAF kwa mwamuzi huyo mpya wakidai itawsaidia Mazembe kwani kocha wao Lamine N’Diaye naye anatoka Senegal. Nusu fainali hiyo ya pili inatarajiwa kuwa ngumu kwa pande zote mbili baada ya timu hizo kutoka sare ya bila ya kufungana katika nusu fainali ya kwanza iliyofanyika jijini Lubumbashi.

No comments:

Post a Comment