Wednesday, October 10, 2012

FA KUANZISHA SHERIA YA KUWABANA WACHEZAJI WATOVU WA NIDHAMU.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, DAVID BERNSTEIN anatarajia kuanzisha sheria mpya kwa ajili ya kudhibiti nidhamu ya wachezaji wa nchi hiyo. Hatua inakuja kufuatia matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu ambayo yameonyeshwa na wachezaji lilikiwemo la ASHLEY COLE ambapo mchezaji atayefunja sheria hiyo anaweza kufungiwa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo. BERNSTEIN amesema kuwa wachezaji wa nchi hiyo wamekuwa kioo cha jamii na vijana wengi wanapenda kufuata ili waweze kupata mafanikio kama yao ndio maana suala la nidhamu ni muhimu ili kuwalinda vijana wengine wanaochipukia wasije kuingia katika mkumbo huo. COLE alijikuta akijiingiza katika matatizo baada ya kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiponda maamuzi ya FA kwa kumchukulia hatua JOHN TERRY. Beki huyo mwenye umri wa miaka 31 alifuta ujumbe huo baadae na kumuomba msamaha BERNSTEIN kabla ya kukutana na PRINCE WILLIAM katika ufunguzi wa kituo kipya cha michezo cha St George Park.

No comments:

Post a Comment