Beki wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Chelsea, ASHLEY COLE anaweza kuepuka adhabu ya kufungiwa baada ya kumuomba msamaha Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA DAVID BERNSTEIN. COLE mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akishitakiwa kufuatia kauli yake ya kuiponda FA kuhusiana na hukumu waliyotoa kwa JOHN TERRY kuhusiana na suala ya ubaguzi wa rangi. BERNSTEIN amesema kuwa mchezaji huyo aliomba radhi siku moja baada ya kutoa kauli hiyo na pia alimuomba radhi wakati alipokutana nae jana usiku kwahiyo haoni haja ya kumchukulia hatua yoyote kwakuwa anajutia alichokifanya. Maamuzi ya kama mchezaji huyo atajumuishwa katika kikosi cha Uingereza katika mchezo wa kufuzu dhidi ya San Marino na Poland yamebakia kwa meneja wa kikosi hicho ROY HODGSON. Akihojiwa kama COLE anaweza kupewa unahodha katika mechi hizo BERNSTEIN alifafanua kuwa FA waliweka wazi toka mwanzo kuwa mchezaji ambaye atakuwa anakiongoza kikosi cha nchi hiyo ni lazima awe na nidhamu ya hali ya juu.
No comments:
Post a Comment