Wednesday, October 17, 2012

KUUMIA KWA ARBELOA NA SILVA KUMECHANGIA SARE - DEL BOSQUE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque anaamini kuumia kwa nyota wake Alvaro Arbeloa na David Silva ndio kulichangia nchi hiyo kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Uafaransa katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Silva ambaye anacheza katika klabu ya Manchester City ya Uingereza alilazimika kutolewa nje katika dakika 13 ya mchezo huo kutokana na kupata matatizo ya misuli wakati Arbeloa ambaye ni beki wa Real Madrid naye aliumia muda mfupi baadae. Del Bosque amesema kuwa kuumia kwa wachezaji hao kulisababisha kikosi chake kushindwa kucheza kama walivyozoea hivyo kusababisha mchezo huo kuwa mgumu lakini pia aliwasifu wapinzani wao kwa kuonyesha soka safi. Hispania inakabiliwa na mechi zingine za kufuzu michuano hiyo Machi 22 mwaka 2013 ambapo wataikaribisha Finland kabla ya kusafiri kuifuata Ufaransa kwa ajili ya mchezo wa marudiano siku nne baadae. 

No comments:

Post a Comment