Tuesday, October 2, 2012

MOURINHO APANGA KUREJEA UINGEREZA.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Jose Mourinho amesema kuwa atarejea Uingereza pindi mkataba wake na klabu hiyo utakapomalizika lakini amesisitiza kuwa ana furaha kuwepo Madrid. Wakati mkataba wa Mourinho ambaye pia amewahi kuinoa Chelsea unaisha mwaka 2016 anafikiri kuwa mkataba mwingine baada ya huo utakuwa katika timu ya Ligi kuu nchini Uingereza. Akihojiwa na kituo cha luninga cha nchini Marekani cha CNN, Mourinho amesema kuwa yeye huwa anapenda kuwa muwazi na kwasababu nyingi alizonazo ataelekea Uingereza baada ya mkataba wake Madrid kumalizika. Mourinho alijiunga Madrid akitokea Inter Milan mwaka 2010 baada kuiwezesha klabu hiyo ya Italia kunyakuwa taji lake la tatu la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment