Tuesday, October 2, 2012
SERENA, VENUS KUZURU NIGERIA.
WANADADA nyota wa kimataifa wa mchezo wa tenisi kutoka Marekani, Serena na Venus Williams wanatarajiwa kufanya ziara barani Afrika katika jiji la Lagos, Nigeria kuanzia Octoba 30 mpaka Novemba 2 mwaka huu. Ziara ya nyota hao ambao ni ndugu ni sehemu ya kampeni ya mpango wa uwezeshwaji kwa wanawake nchini humo mpango ambao tayari umefanikiwa na kuungwa mkono kimataifa. Kama wanavyofanya Marekani na sehemu zingine duniani wakati watakapokuwa Lagos nyota hao wanatarajiwa kuvutia, kuhamasisha na kutoa ushauru kwa mapama katika chakula cha jioni, kliniki na mechi za maonyesha ambazo zitakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya ziara wanadada hao. Ziara ya wanadada hao inatarajiwa kuongeza chachu juu ya jukumu ushiriki wa wanawake katika kuhimiza, kuhamasisha na kutoa mitizamo yao katika maendeleo barani Afrika. Pia hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa wanadada hao kuchuana wenyewe kwa wenyewe katika tenisi kwenye ardhi ya Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment