Tuesday, October 16, 2012

MWESINGWA AOMBA RADHI KUFUATIA KUTOLEWA KWA CRANES.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Uganda Cranes, Andy Mwesingwa ameomba radhi kwa taifa na mashabiki wa soka nchini humo kwa kushindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo itafanyika nchini Afrika Kusini 2013. The Cranes walifanikiwa kuwafunga Zambia maarufu kama Chipolopolo bao 1-0 katika muda wa kawaida mwishoni mwa wiki iliyopita lakini waliotolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-9 baada ya kumaliza kwa sare. Mwesigwa alikosa mojawapo ya penati mbili za Uganda huku Patrick Ochan naye akishuhudia penati yake ikizuiwa na kipa wa Chipolopolo Kennedy Mweene na kuwafanya mabingwa hao wa Afrika kukata tiketi ya kwenda kutetea kombe lao katika michuano hiyo. Mwesingwa amesema katika suala la upigaji penati hakuna mchezaji ambaye anaweza kutamba kwamba yeye ni mjuzi zaidi haswa mchezo kama ule hivyo kukosa kwake kuchukuliwe kama ni bahati mbaya na kuomba mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwa ajili ya ajili ya mashindano mengine yaliyopo mbele yao.

No comments:

Post a Comment