Tuesday, October 30, 2012

NINA NDOTO ZA KUSTAAFU SOKA NIKIWA BARCELONA - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa ana ndoto za kustaafu kucheza soka akiwa katika klabu hiyo ambayo imemfundisha toka mdogo na kuanza rasmi kucheza soka la kulipwa 2004. Kauli ya nyota huyo imekuja wakati akipokea tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyopewa kufuatia kuongeza orodha ya wafungaji barani Ulaya msimu uliopita akiwa na mabao 50. Messi aliishukuru Barcelona kwa kumoa nafasi ya kutambua kipaji chake wakati walipomchukua katika shule yao ya michezo akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2000. Messi mwenye umri wa miaka 25 sasa ana mkataba wa miaka minne ambao una thamani ya paundi milioni 250 na maofisa wa klabu hiyo wamesema kuwa wako tayari kuuboresha zaidi mkataba huo. Mpaka sasa nyota huyo ameshafunga mabao 270 kwa klabu yake hiyo na 31 kwa timu ya taifa ya Argentina. 

No comments:

Post a Comment