Tuesday, October 30, 2012

WAZIRI MKUU SENEGAL AMTAKA RAIS WA FSF KUJIUZULU.

WAZIRI Mkuu wa Senegal, Abdoul Mbaye amemtaka rais wa Shirikisho la Soka la Senegal-FSF Augustin Senghor kujiuzulu wadhfa wake huo kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya nchi hiyo na Ivory Coast. Maofisa watatu wa juu wa shirikisho hilo walijiuzulu Jumatatu ikiwa ni wiki moja toka makamu wa rais Lamotte Louis kujitoa katika kamati ya utendaji baada ya kukubali kuwajibika kwa vurugu zilizotokea uwanjani. Hatahivyo, Senghor alikataa kujiuzulu baada ya kujitetea kuwa serikali ilikuwa ikiingilia mambo yao ya michezo. Akihojiwa Senghor amesema kuwa haoni haja ya kujiuzulu kwani hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kuwalazimisha kujiuzulu kwasababu walichaguliwa kihalali na muda wao wa kukaa madarakani bado haujakwisha. Senghor aliendelea kusema kuwa ataitisha mkutano wa dharura kesho kwa wajumbe 23 wa kamati ya utendaji waliobakia ili kuziba pengo la wajumbe wanne waliojiuzulu.

No comments:

Post a Comment