Sunday, October 28, 2012

KUVUNJA REKODI YA PELE SIO MUHIMU KWANGU - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa kuvunja rekodi ya Pele kwa kufunga mabao mengi zaidi katika mwaka mmoja haina umuhimu sana kwake kulinganisha na kuisaidia timu yake kupata mafanikio zaidi. Messi alifunga mabao mawili na kufikisha mabao 73 kwa mwaka huu katika mchezo dhidi ya Rayo Vallecano jana na kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwafikia nguli wa zamani Pele ambaye alifunga mabao 75 na Gerd Mullaer aliyefunga mabao 85. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi amesema kuwa kuvunja rekodi ya Pele sio suala la umuhimu sana kwake kwani wameshinda mchezo huo katika mazingira magumu na hilo ndio suala la umuhimu zaidi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kupewa kiatu chake cha dhahabu Jumatatu baada ya kumaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora Ulaya ambapo aliwashukuru wachezaji wenzake kwani bila wao asingeweza kupata zawadi hiyo.

No comments:

Post a Comment