Sunday, October 28, 2012

NITAKUWA MVUMULIVU KWA WILSHERE - WENGER.

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema atakuwa mvumilivu juu ya ujio Jack Wilshere baada ya kiungo huyo kucheza mechi yake ya kwanza baada ya miezi 17 wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Queens Park Rangers jana. Wilshere ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na kifundo cha mguu alicheza kwa dakika 67 katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Emirates baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza pasipo kutegemewa na Wenger. Wenger alionyesha kufurahishwa na kiwango alichokionyesha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza baada ya kuweka wazi kuwa hakumwambia Wilshere kama atacheza mchezo huo mpaka asubuhi. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa atakuwa akimtumia mchezaji huyo kwa tahadhari wakati akiendelea kurejea katika kiwango chake cha kawaida na amemuondoa katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa Kombe la Ligi dhidi Reading katikati ya wiki hii.

No comments:

Post a Comment