Sunday, October 28, 2012

MECHI YA MAHASIMU YA LUPOPO NA MAZEMBE YASOGEZWA MBELE KUTOKANA NA VURUGU.

WATU watano wakiwemo polisi wawili wameumia vibaya wakati vurugu zilipozuka kabla ya mchezo wa Jumamosi jijini Lubumbashi ambao unawakutanisha mahasimu wawili timu za Saint-Eloi Lupopo na TP Mazembe mchezo ambao uliahirishwa kutokana na vurugu hizo. Taarifa ya polisi imesema kuwa maofisa wawili wa polisi na mashabiki watatu ndio walioumia sana lakini wapo mashabiki wengine wengi ambao walipata majeraha ya kawaida katika kdhia hiyo. Mashuhuda wanasema kuwa vurugu hizo zilizuka wakati mashabiki wa timu zote mbili walipoanza kurushiana mawe kabla ya polisi kuingilia na kuwarushia mabomu ya machozi ili kujaribu kutuliza vurugu hizo. Matukio ya vurugu sasa imeonekana kuwa kama tabia za kawaida kwa mashabiki wa soka barani Afrika baada ya kutokea kwa matukio ya aina hiyo mara kwa mara huku mengine yakichukua maisha ya watu.

No comments:

Post a Comment