Sunday, October 28, 2012

LORENZO BINGWA MICHUANO YA MOTOGP.

DEREVA nyota wa mashindano ya pikipiki, Jorge Lorenzo amejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la pili la dunia la michuano ya MotoGP baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya michuano ya Australian GP. Casey Stoner wa Autralia ndio aliyeshinda mbio hizo zilizofanyika katika kisiwa cha Philip kwa mara sita mfululizo lakini dereva mwenzake kutoka timu ya Respol Honda, Dani Pedrosa akipata ajali katikati ya mashindano hayo. Pedrosa ambaye alikuwa akihitaji kumaliza mbele ya mhispania mwenzake Lorenzo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la dunia katika mashindano hayo ya mwisho kwa maka huu alipata ajali katika mzunguko wa pili. Lorenzo ambaye ni dereva wa Yamaha mara ya kwanza alishinda taji la dunia mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment