Monday, October 1, 2012

NYAMILANDU ANUSURIKA KATIKA AJALI.

RAIS wa Chama cha Soka nchini Malawi-FAW, Walter Nyamilandu amenusurika katika ajali mbaya ya gari ambayo imewaua mchumba wake mtarajiwa Maria Inglis na shangazi yake ajali ambayo ilitokea Juzi. Nyamilandu ambaye alitibiwa na kuruhusiwa katika hospitali ya wilaya ya Balaka nchini humo alikuwa akiendesha gari aina na Nissan Pathfinder akitokea Blantyre kuelekea Lilongwe. Ajali hiyo ilimkuta katika eneo la Phalula ambapo gari hilo lilipinduka ambapo taarifa za kwanza za polisi zinasema kuwa alikuwa akijaribu kulikwepa roli ambalo inaonekana lilikuwa limekosa mwelekeo. Katika ajali hiyo watoto wawili wa Nyamilandu nao pia walitoka salama, ambapo sasa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kugundua haswa chanzo cha ajali hiyo ambaya.

No comments:

Post a Comment