Monday, October 1, 2012

ETO'O AREJEA KUIOKOA CAMEROON.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o amerejea rasmi katika katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo. Eto’o ambaye katika kipindi cha karibuni alitangaza kupumzika kuitumikia Cameroon alithibitisha kubatilisha uamuzi wake huo hivyo hiyo inamaanisha kuwa mchezaji ambaye ndiye anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwasasa atakuwepo katika mchezo wa kufuzu mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde mchezo ambao utapigwa jijini Younde Octoba 14 mwaka huu. Mcheaji ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne amesema kuwa katika kipindi cha karibuni amekuwa akipokea wageni ambao ni maofisa wa soka nchini kwake kuzungumzia masuala ya soka la nchi hiyo hususani mustakabali wa timu ya taifa. Eto’o amesema mbali na viongozi hao wa soka lakini pia rais wan chi hiyo na Waziri Mkuu nao pia walimfuata kuzungumzia suala hilo na kupelekea kubadilisha mawazo na kurejea katika kikosi hicho ili kujaribu kunusuru soka la nchi ambalo katika kipindi cha karibuni limekuwa kama halina muelekeo. Kocha mpya wa kikosi hicho Jean Paul Akono aliweka wazi toka akipewa kibarua hicho kuwa lazima awajumuishe Eto’o na beki wa kushoto wa timu ya Tottenham Hotspurs Benoit Assou Ekotto katika kikosi chake ambapo kitakuwa kikisaka ushindi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment