Wajukuu wa malkia ELIZABETH wa pili wa Uingereza, PRINCE WILLIAM na mkewe KATE MIDDLETON wanatarajiwa kufungua kituo kipya cha michezo kiitwacho St George Park kilichopo Staffordshire. Kituo hicho kilichogharimu paundi milioni 105 ambapo PRINCE WILLIAM atakuwa rais wake kinatarajiwa kuinua kiwango cha soka nchini Uingereza kwa rika zote. Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA, DAVID BERNSTEIN amesema kuwa matarajio waliyonayo yatawezekana kutokana na kuwapa mafunzo zaidi na bora makocha wa soka ambao watapewa jukumu la kuwafundisha soka vijana wa rika mbalimbali nchini humo. Kituo hicho mbali na kutoa mafunzo kwa makocha lakini pia kitashughulika na mambo ya matibabu ya michezo, sayansi ya michezo pamoja na masuala ya ushauri nasaha.
No comments:
Post a Comment