Wednesday, October 10, 2012

ABIDAL AANZA MAZOEZI.

Beki wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Barcelona, ERIC ABIDAL ameanza mazoezi katika milima ya Pyrenees nchini Hispania baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine April mwaka huu. Katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Barcelona, ABIDAL mwenye umri wa miaka 33 ameanza mazoezi hayo chini ya mwalimu wa viungo wa klabu hiyo EMILI RICART ambaye amekuwa mazoezi mbalimbali ili kumrejesha katika kiwango chake. 
Kabla ya upasuaji wa kupandikiza ini jingine Abidal alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe katika ini Machi mwaka 2011 kabla ya kurejea uwanjani miezi miwili baadae na kuisaidia timu yake kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Manchester United katika fainali iliyochezwa jijini London. Baadae madaktari waliamua kuwa ABIDAL ambaye kucheza katika vilabu vya Minaco na Olympique Lyon anahitaji kupandikizwa ini jingine ambapo mara baada ya upasuaji huo uliokuwa wa mafanikio nyota huyo alisema kuwa anategemea kurejea uwanjani tena Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment