Wednesday, October 10, 2012

BUSQUETS AFUNGIWA MECHI MBILI UEFA.

Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA limemfungia michezo miwili kiungo nyota wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona SERGIO BUSQUETS. Adhabu hiyo imekuja kufuatia mchezaji huyo kutolewa nje katika dakika ya 88 ya mchezo baina ya timu yake dhidi ya Benfica wiki moja iliyopita baada ya kuonyesha mchezo usiokuwa wa kiungwana. Kufungiwa kwa mchezaji huyo itakuwa ni pigo kubwa kwa klabu hiyo ambayo katika siku za karibuni mabeki wake wa kati tegemeo wamekuwa majeruhi na kupelekea BUSQUETS kuwa ndio mbadala wao katika kucheza nafasi hiyo. BUSQUETS anatarajiwa kukosa michezo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Celtic katika kundi G, lakini klabu hiyo imepewa siku tatu kupinga adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment