Wednesday, October 10, 2012
KAKA KUCHEZA MECHI YA BRAZIL NA IRAQ.
Kiungo nyota wa kimataifa wa Brazil, KAKA anaweza kuwemo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Iraq kesho, ikiwa ni mara ya kwanza mchezaji kurejea katika kikosi hicho toka michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010. Kiungo huyo ambaye pia anakipiga katika klabu ya Real Madrid alionekana akifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha kwanza cha nchi hiyo kama OSCAR na washambuliaji HULK na NEYMAR wakijiandaa na mchezo huo. Kocha wa Brazil MANO MENEZES alibainisha kuwa anaweza kumtumia Kaka katika nafasi ya kiungo ingawa OSCAR anayecheza katika klabu ya Chelsea ndio amekuwa akicheza nafasi hiyo kwenye kikosi hicho hivi sasa. Mchezo wa mwisho KAKA kuichezea Brazil ulikuwa ni dhidi ya Uholanzi katika robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini ambapo Brazil walitolewa. MENEZES pia amemjumuisha ADRIANO katika kikosi chake hicho kuziba pengo la DANIEL ALVES ambaye ameachwa kutokana na kuwa majeruhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment