Wednesday, October 24, 2012

RADWANSKA, WILLIAMS, SHARAPOVA WAANZE WTA CHAMPIONSHIP, ISTABUL.

WACHEZAJI nyota wa tenisi Agnieszka Radwanska, Serena Williams na Maria Sharapova wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kushinda michezo yao katika michuano ya WTA inayofanyika jijini Istabul, Uturuki. Radwanska alifanikiwa kusonga mbele baada ya kumfuga bingwa mtetezi wa michuano hiyo Petra Kvitova kwa 6-3 6-2 wakati Williams wa Marekani alimfunga Angelique Kerber wa Ujerumani kwa 6-4 6-1. Sharapova wa Urusi alimsambaratisha tena kama alivyofanya katika michuano ya wazi ya Ufaransa Sara Errani wa Italia kwa 6-3 6-2 huku Victoria Azarenka Belarus na Li Na wa China nao wakitarajiwa kujitupa uwanjani kwa nyakati tofauti baadae leo. Michuano hiyo ambayo ni ya mwisho kwa mwaka huu inajumuisha wanadada nane ambao wanashika nafasi ya juu katika orodha za ubora duniani ambapo wamegawanywa katika makundi mawili huku kila kundi likitoa wachezaji wawili ambao watachuana katika nusu fainali na baadae fainali.

No comments:

Post a Comment