Wednesday, October 24, 2012

PAMOJA NA VURUGU ZILIZOTOKE SENEGAL YAINGIZA DOLA 300,000 KATIKA MCHEZO BAINA YAKE NA IVORY COAST.

KITENGO cha fedha cha Shirikisho la Soka nchini Senegal-SFF kimetangaza mapato ya dola 300,000 katika mchezo baina ya nchi hiyo na Ivory Coast pamoja na vurugu zilizotokea na kusababisha mchezo kumalizika kabla ya muda wake wa kawaida. Uwanja wa Leopold Sedar Senghor uliopo jijini Dakar ulikuwa umesheheni mashabiki zaidi ya 60,000 wengi wakiwa wenyeji ambao baadhi yao walianza kurusha vitu mbalimbali uwanjani baada ya timu yao kufungwa bao la pili na kuwepo matumaini madogo ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013. Mwamuzi wa mchezo huo ilibidi amalize mchezo huo dakika ya 74 baada ya vurugu kuongezeka ambapo baadaye Shirikisho la Soka la Afrika-CAF liliipa ushindi wa mabao 2-0 ambao Ivory Coast waliupata. Serikali ya Senegal iliomba msamaha kwa watu wa Ivory Coast pamoja na wadau wa soka kwa tukio hilo huku wakipeleka matokeo ya uchunguzi wao CAF kwa ajili ya hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment