Wednesday, October 24, 2012

WAZIRI WA MICHEZO POAND AJIUZULU.

Anna Mucha.
WAZIRI wa Michezo nchini Poland amejiuzulu kufuatia kuahirishwa kwa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Uingereza wiki iliyopita baada ya mvua iliyonyesha kujaza maji katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA liliamuru mchezo huo kuchezwa siku moja baadae wakati maofisa wa soka wa nchi hiyo waliposhindwa kufunga paa la uwanja huo ambao umegharimu kiasi cha dola milioni 550 kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012. Mashabiki na wadau wa soka wa nchi hiyo wamekuwa wakiponda uzembe uliofanyika na kumtaka Waziri Mkuu Donald Tusk kuwawajibisha wale wote waliohusika na uzembe huo. Waziri wa Michezo Anna Mucha aliwaambia waandishi wa habari kuwa akiwa kama mwanasiasa anaona anawajibika kwa namna moja au nyingine kwani jukumu la waziri ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa. Waandaaji wa mchezo huo wameema kuwa paa la uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 58,000 lilishindwa kufungwa kutokana na sababu za kiusalama na sio timu wala FIFA waliokuwa wakitaka paa hilo lifungwe wakati mvua ikinyesha.

No comments:

Post a Comment