Wednesday, October 24, 2012

UNITED YASUBIRI MKATAB MNONO WA NIKE.

Add caption
KLABU ya Manchester United wanatarajia kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na kampuni kongwe ya vifaa vya michezo ya Nike Februari mwakani baada ya mkataba wao wa awali ambao una thamani ya paundi milioni 303 kukaribia kumalizika mwaka 2015. Ofisa Mkuu wa United Ed Woodward anatarajia kuanza mazungumzo na kampuni hiyo ambayo yatachukua muda wa mizei sita kuangalia uwezekano wa kampuni hiyo kuongeza fedha zaidi katika mkataba mpya. Kampuni nyingi zimekuwa zikifukuzia kusaini mktaba wa udhamini kwa timu hiyo katika kipindi cha miaka sita kuanzia Vodafone ambao walisaini mkataba wa paundi milioni nane mpaka Chevrolet waliosaini mkataba wa paundi milioni 52 kwa mwaka kuanzia mwaka 2014-2015. Kwa kutegemea hali hiyo United wanategemea Nike kuongeza fungu hilo kutoka kiasi cha paundi milioni 303 kwa mwaka mpaka paundi bilioni moja katika mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment