Sunday, October 21, 2012

UAMUZI WA MURRAY KUMCHUKUA ROBSON BADALA YANGU ULINIONGEZEA CHANGAMOTO YA KUFANYA VIZURI ZAIDI - WATSON.

MWANADADA nyota katika mchezo wa tenisi, Heather Watson ameweka bayana kuwa hakufurahishwa na uamuzi wa Andy Murray kumchukua Laura Robson katika michuano ya tenisi ya olimpiki ya wawili wawili iliyofanyika London mwaka huu. Katika michuano hiyo Murray na Robson waliambulia medali ya fedha lakini Watson mwenye umri wa miaka 20 amesema kuachwa huko ndiko kulikomfanya ajifue zaidi na kunyakuwa taji lake la kwanza la Grand Slam la michuano ya wazi ya Japan iliyofanyika jijini Osaka. Watson amesema kuwa michuano ya olimpiki ni ya kipekee na kila mtu angependa kucheza lakini ulikuwa ni uamuzi wa Murray kumchagua Robson kama mchezaji mwenza na kumaliza michuano hiyo na medali ya fedha kitu ambacho ni kizuri kwasababu wamewakilisha vyema waingereza. Ushindi wa Watson wa michuano hiyo ya Japan umemuingiza katika orodha za wachezaji 50 bora wa mchezo huo kwa upande wa wanawake nafasi mbili nyuma ya Robson lakini mwanadada huyo bado anaonyesha kiu ya kupata mafanikio zaidi huko mbele.

No comments:

Post a Comment