Sunday, October 14, 2012

WATSON ANYAKUWA MICHUANO YA WAZI YA JAPAN.

MCHEZA tenisi Heather Watson anakuwa mwanadada wa kwanza wa Uingereza kushinda taji la WTA toka mwaka 1988 baada ya kufanikiwa kumfunga Kai-Chen Chang katika mchezo wa fainali ya michuano ya wazi ya Japan. Watson ambaye anashika namba 71 katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake alifanikiwa kumfunga Chang raia wa Taipei ambaye anashika namba 134 kwa seti 2-1 zenye alama za 7-5 5-7 7-6. Watson pia amefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya wawili wawili akiwa na Kimiko Date-Krumm ambapo watacheza na Abigail Spears na Raquel Kops-Jones wa Marekani. Ushindi huo wa Watson aliopata jijini Osaka unakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya mwingireza mwenzake Laura Robson kutinga fainali ya michuano ya wazi ya Guangzhou iliyofanyika China na kuwa mwanamke wa kwanza nchini Uingereza kutinga fainali ya michuano ya WTA toka Jo Durie alipofanya hivyo mwaka 1990.

No comments:

Post a Comment