Sunday, October 14, 2012

MCHEZO WA SENEGAL NA IVORY COAST WASHINDWA KUMALIZIKA KUTOKA NA VURUGU.

MCHEZO muhimu wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Ivory Coast ulitelekezwa baada ya mashabiki kuanzisha vurugu uwanjani jijini Dakar. Mashabiki wa Senegal walianza kuwasha moto katika majukwaa na kutupa vitu mbalimbali uwanjani baada ya kushuhudia timu yao ikifungwa mabao 2-0 matokeo ambayo yanamaanisha timu yao kushindwa kufuzu michuano hiyo. Mashabiki wa Ivory Coast walilazimika kuruka na kukimbilia uwanjani kuepuka vurugu zilizokuwepo ambapo waliungana na wachezaji wao na kuondolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa polisi. Taarifa zinasema kuwa watu 10 akiwemo Waziri wa Michezo wa Senegal Hadji Malick Gakou waliumizwa katika vurugu hizo zilizotokea katika Uwanja wa Leopold Sedar Senghor. Vurugu zilizuka baada ya mshambuliaji nyota wa Ivory Coast Didier Drogba kufunga bao la pili kwa penati zikiwa zimebakia dakika 15 kabla ya mpira kumalizika.

No comments:

Post a Comment