Friday, November 16, 2012

BARCELONA KUVAA QATAR AIRWAYS MSIMU UJAO.

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania inatarajia kubadilisha wadhamini wa jezi zao msimu ujao na kuvaa jezi za Qatar Airways kama mdhamini wao rasmi wa jezi zao. Nembo hiyo ya shirika la ndege itachukua nafasi ya Qatar Foundation nembo ambao ndio inayoonekana katika fulana zao msimu huu. 
Mabadiliko hayo ni sehemu ya makubaliano ya udhamini yenye utata ambayo yalisainiwa na Kampuni ya Michezo ya Uwekezaji ya Qatar-QSI mwaka uliopita. Barcelona ilisaini mkataba huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikuwa mkataba wenye faida kubwa katika mchezo wa soka ambao ulikuwa na thamani ya euro milioni 30 kwa mwaka pamoja na kuitangaza nchi hiyo ambayo itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Kabla ya kuvaa jezi zenye nembo ya Qatar Foundation Barcelona walikuwa wakivaa nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulika na masuala ya watoto-UNICEF ambapo kwasasa nembo hiyo imehamishwa kwa nyuma ya jezi za klabu hiyo. Barcelona walikuwa wakiwalipa UNICEF euro milioni 1.5 kwa mwaka kwa kutumia jina hilo kwenye jezi zao.

No comments:

Post a Comment