Thursday, November 1, 2012

DJOKOVIC ASHINDWA KUTAMBA PARIS MASTERS.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Serbia, Novak Djokovic ameshindwa kutamba katika michuano ya Paris Masters na kujikuta akitolewa na Sam Querrey wa Marekani katika mzunguko wa pili. Djokovic ambaye ana uhakika wa kumaliza mwaka akiwa katika nafasi ya kwanza ya orodha za wachezaji bora wa mchezo huo dunia alianza vyema baada ya kushinda seti ya kwanza bila kupoteza alama lakini alijikuta akishindwa kuendelea kufanya vizuri katika seti zingine na kufungwa kwa 0-6 7-6 6-4. Djokovic anayeshika namba mbili ambaye anatachukua nafasi ya kukaa namba moja ambayo inashikiliwa na Roger Federer pamoja na kupoteza mchezo huo ka Querrey alitinga uwanjani jijini Paris akiwa amevaa kinyago cha Vader Mask kuazimisha sherehe za Halloween. Katika michezo mingine ya iliyochezwa jana David Ferrer ambaye ndiye mchezaji pekee aliyekuwepo katika orodha za juu, Juan Monaco na Janko Tipsarevic walishinda michezo yao na kuinga mzunguko wa tatu wa michuano hiyo ya mwisho kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment