Saturday, November 10, 2012
FIFPRO YAPINGA KUANZISHWA UMOJA WA WACHEZAJI WEUSI.
KATIBU Mkuu wa Muungano wa Wachezaji Duniani-FIFPro, Theo van Seggelen amesema kuwa haina mantiki kuanzisha muungano tofauti kwa wachezaji weusi. Jumuiya ya Mawakili Weusi imesema kuwa iko katika mazungumzo ya kuanzisha muungano mpya wa wachezaji weusi ili kutetea haki zao ikiwemo suala la ubaguzi wa rangi ambalo limekuwa likiota mizizi katika siku za karibuni. Lakini Seggelen amesema kuwa FIFPro inaheshimu wachezaji wote iwe ni kutoka ligi daraja la tatu nchini Uingereza, Cina au Congo hivyo haitaleta mantiki kama wakiunda umoja mwingine wa wachezaji weusi. Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini Uingereza-PFA ni wajumbe wa FIFPro muungano ambao unawakilisha wachezaji wapatao 60,000 dunani nzima hivyo Seggelen anadhani umoja huo hautakuwa na maana kama wachezaji weusi wakianzisha umoja wao. Segellen amesema kuwa kama unalinda haki za wachezaji wa kulipwa wapatao 60,000 huwezi kuwatofautisha kati ya mweusi au mweupe au Muislamu au Mkristo au ni tajiri au maskini kwani falsafa yao ni haki sawa kwa wachezaji kitu katika ngazi za kimataifa sio kitu rahisi. Mwenyekiti wa PFA Clarke Carlisle naye pia alipinga kuanzishwa kwa umoja akidai kuwa unaongeza mgawanyiko na kitarudisha nyuma juhudi za kupingana na ubaguzi wa rangi zinaondelea hivi sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment