Thursday, November 8, 2012

INTER, PARTIZAN, LYON, LEVERKUSEN, KAZAN, METALIST NA HANOVER 96 ZATINGA 32 BORA EUROPA LEAGUE.

MABAO mawili yaliyofungwa na Rodrigo Palacio yaliiiwezesha Inter Milan kutinga katika hatua ya mtoano wa Europa League wakati Atletico Madrid walijikuta wakifungwa kwa mara ya kwanza katika mechi 16 walizocheza nchini Ureno. Milan ambao waliwafunga Partizan Belgrade ya Serbia kwa mabao 3-1 wameungana na timu za Bayer Leverkusen, Rubin Kazan, Metalist Kharkiv, Hanover 96 na Olympique Lyon katika hatua hiyo ya mtoano ambayo itashirikisha timu 32. Rubin Kazan ya Urusi ilifanikiwa kuongoza katika kundi H wakiwa na alama 10 sawa na Inter baada ya kuifunga Neftchi Baku ya Azerbaijan kwa bao 1-0 wakati Leverkusen na Metalist nazo pia zikikabana koo kwa alama 10 katika kundi K baada ya kushinda michezo yao ya jana usiku. Lyon waliendeleza rekodi yao nzuri kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mshindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Athletic Bilbaona kushika usukani wa kundi I wakifuatiwa na Sparta Prague katika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment