Thursday, November 8, 2012

MUAMBA AWASHUKURU MASHABIKI WA WHITE HART LANE.

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Bolton Wanderers, Fabrice Muamba ambaye alikumbwa na tatizo la moyo wake kusimama wakati wa mchezo baina ya timu yake na Totenham Hotspurs Machi mwaka huu amerejea kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa White Hart Lane mahali ambao ndipo alipoanguka. Muamba ambaye moyo wake ulisimama kwa dakika 78 baada ya kuanguka wakati wa mchezo huo wa Kombe la FA baadae alipona kabisa kutokana na tatizo hilo lakini alilazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 24 kutokana na ushauri wa madaktari. Akitembea uwanjani wakati wa kipindi cha mapumziko katika mchezo wa Europa League kati ya Spurs na Maribor ya Slovenia, Muamba alionyesha mahali ambapo alianguka na baade kuzungumza na mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo. Muamba aliwashukuru mashabiki wa Spurs ambao walikuwepo na kumuombea wakati alipopata tatizo hilo na kusema kwamba hatawasahau kamwe katika maisha yake. Timu ya madaktari wa Spurs na Bolton walijaribu kuokoa maisha ya Muamba kwa muda wa dakika 20 baada ya kuanguka kabla ya kuondolewa na ukimbizwa hospitali ambapo alilazwa kwa kipindi cha wiki nne.

No comments:

Post a Comment