Thursday, November 8, 2012

VIWANJA SITA KUWA TAYARI KWA AJILI YA CONFEDERATION CUP JUNE MWAKANI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema kuwa viwanja sita kama vitakuwa tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kama ilivyopangwa mwanzoni. Katika taarifa yake iliyotolewa jana imeelezea kuwa miji iliyopo Kaskazini-Mashariki ya Salvador na Racife itakuwa miji mojawapo itakayoandaa michuano hiyo ambayo itafanyika mwakani huku mingine ikiwa ni miji ya Rio de Janeiro, Brasilia, Salvadr na Fortaleza. Pamoja na kutangaza miji hiyo sita ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo lakini Recife na Salvador itathibitishwa rasmi kama wakionyesha jitihada na kulishawishi shirikisho hilo kwamba maandalizi yao yatakamilika kwa wakati. Kombe la Shirikisho litaanza kutimua vumbi June 15 hadi 30 mwakani ambapo itazikutanisha nchi sita ambazo ni mabingwa wa mabara, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na nchi wenyeji wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment