Thursday, November 8, 2012

KIKOSI CHA TAIFA CHA NGUMI KITAKACHOPAMBANA NA ZAMBIA.

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeidhinisha jumla ya wachezaji saba waliochaguliwa na makocha wa timu ya taifa katika mashindano maalum yaliyofanyika tarehe 6/11/2012 mwenge Dar es salaam. Wachezaji waliochaguliwa na kuidhinishwa kuwakilisha timu ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Zambia na uzito wao ni:- 
1. Said Hofu 49 Kgs Light Fly 
2. Amdani Issa 52 Kgs Fly Weight 
3. Frank Nicolas 56 Kgs Bantam 
4. Ismail Galiatano 60 Kgs Light Weight 
5. Kassim Hussein 64 Kgs Light Welter 
6. Mohamed Chibumbui 69 Kgs Welter Weight 
7. Gulushid Rashid 75 Kgs Middle. 
Jumla ya wachezaji 15 wanaendelea na mazoezi uwanja wa ndani wa taifa chini ya makocha Juma Selemani, Said Omari na Mussa Maisori. Mashindano ya kimataifa ya Tanzania na Zambia yatafanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo tarehe 10/11/2012 kuanzia saa 9.00 Alasiri. Lengo la mashindano hayo ni kuipatia timu yetu taifa uzoefu wa kaimataifa kabla ya kushiriki mashindanao makubwa ya kimataifa kama ya Jumuiya ya Madola ,mashindano ya Afrika na Olimpiki. Wito kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yetu ya Tanzania kwa kuchangia kiingilio cha Tsh 10,000/= kwa Tsh 5,000/=. Aidha taarifa kutoka shirikisho la ngumi la Zambia iliyotumwa na Rais wa shirikisho la ngumi Zambia ndugu Thomas Chileshe zimeeleza kuwa wachezaji wa zambia wameondoka leo kwa njia ya barabara na kesho wanatarajia kufika Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment