Wednesday, November 7, 2012

HULK, ADRIANO KUIKOSA COLOMBIA.

SHIRIKISHO la Soka la Brazil limesema kuwa mshambuliaji wa Zenit St. Petersburg , Hulk na beki wa Barcelona Adriano hawatajumuishwa katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia wiki ijayo jijini New Jersey, Marekani. Shirikisho hilo limesema kuwa wachezaji hao wameachwa kutokana nakuwa majeruhi baada ya kuumia wakati wakitumikia vilabu vyao katika mechi za ligi. Mchezo huo wa kirafiki ambao utafanyika katika Uwanja wa MetLife utakuwa ni mchezo mwisho kwa Brazil kwa mwaka huu lakini pia utakuwa mchezo wa 1,000 katika historia ya klabu hiyo. Kocha wa Brazil Mano Menezes pia atawakosa nyota wengine ambao ni beki wa Real Madrid Marcelo, Alex Sandro anayecheza Porto na Dede anayekipiga katika klabu ya Vasco da Gama.

No comments:

Post a Comment