Saturday, November 17, 2012
MADEREVA WA LANGALANGA WASIFU BARABARA ZA AUSTIN, TEXAS.
MADEREVA wa mashindano ya magari yaendayo kasi ya Langalanga wamesifu barabara za Austin, Texas ambako kunafanyika mashindano ya Grand Prix ya Marekani. Dereva wa McLaren ambaye msimu ujao anahamia Marcedes, Lewis Hamilton alisifu barabara hizo ambazo zimejengwa katika siku za karibuni na hayo yakiwa mashindano yake ya kwanza. Madereva wengine waliosifia barabara hizo ni Jenson Button ambaye wanatoka timu moja na Hamilton akidai kuwa unaweza kukimbia kwa kasi na kukata kona ukiwa katika kasi kubwa bila kuteleza kitu ambacho kwenye barabara nyingine huwezi kufanya. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo ambapo Sebastian Vettel wa timu ya Red Bull anatarajiwa kuongoza mbio hizo baada ya kufanikiwa kuendesha kwa kasi zaidi katika mbio za majarabio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment