Wednesday, November 14, 2012

PELE ALAZWA.

Msemaji wa kituo cha afya cha Albert Einstein amesema kuwa mchezaji nguli wa zamani wa soka Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amelazwa katika kituo hicho kilichopo jijini Sao Paulo. Msemaji huyo alithibitisha hayo lakini alikataa kuelezea kwa undani zaidi kinachomsumbua nyota huyo mwenye umriwa miaka 72 ikiwa ni shinikizo kutoka kwa familia yake ambao hawakutana ugonjwa unaomsumbua nyota huo kuwekwa wazi. Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la Folha de Sao Paulo nyota huyo ambaye pia anajulikana kwa jina la utani la The King au Mfalme aliripotiwa kufanyiwa upasuaji wa nyonga. Pele anahesabiwa kama mmoja wapo ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika mchezo wa soka akiwa ameshinda Kombe la Dunia katika vipindi vitatu tofauti mwaka 1958, 1962 na 1970 huku akiwa amefunga mabao 1,281 katika kipindi chote alichosakata kabumbu.

No comments:

Post a Comment